Usiset target ya kuishi Runda na huwezani

Photo:Courtesy

Mwaka wa 2016 imepita, na ndio sasa tunasema kwaheri kwa hiyo mwaka.

Sasa tunakaribisha 2017 na tunasema ni asante sana kwa Sir Jah kutufikisha hapo. Tunajua watu wengi sana wangependa kukemba hii December ya 2016 lakini hawajaiona.

Ndio maana kama uko uhai ukae ukijua ya kwamba kujisundia target kwa life ni kitu ya maana sana na raiya mob haijuangi hivyo. Wale wanajua nao huset target zao vibaya, wengine huset target zao saa zile wako kazi

— lakini kazi ikiisha wanasahau walikua wamejisetia target.

Watu wengi huset target zao mwaka ikiisha ama ikianza, na kuna wengine hujisetia target siku yao ya birthday

— juu mwaka ya mtu huanza saa zile alizaliwa. Watu wengi husema eti New Year huanza January, but mwaka mpya huanzia mtu saa zile anacelebrate birthday yake

— na hiyo ndio time poa ya kujisetia target yako ya mwaka.

Targets ni za aina mob, kuna watu hujisetia target ya kuoa. Unaskia mtu akisema eti by next year August atakua ameoa na amepata mtoto mmoja. Wengine huset target eti by next year sitakua nimeandikwa job, nitakua self employed. Wengine wameset target ya kujenga nyumba, wengine ni target za kuhama kuishi na wazazi wao, wengine ni target eti by 2017 hawatakuwa wanavuta fegi tena

— yaani kila mtu hukua na target yake, but kufulfill hiyo target ndio inakuanga kizungumkuti. Kuset target na kuitimiza ndio huwanga ni blanda.

Watu wengi huset target zao December, eti wakianza 2017, mambo ikue ital kwao

— ndio maana nawaambia ukijisetia target jisetie ile target unajua unawezana nayo. Kumbuka target zingine zinafanyanga watu washikwe na stress na hata wengine kufyatuka. Huwezi jisetia target ya kuishi Karen ama Runda by March na saa hizi unaishi Korogocho na hauna kazi.

Huwezi jisetia target ya kuoa na bado unaishi na mama yako. Huwezi jisetia target ya kuacha wizi na bado unasema hii ndio mwezi yako ya mwisho kuibia watu.Life yako ni wewe, na ndio maana ukijisetia target jisetie wewe mwenyewe juu watu wengi hujisetia target kulingana na mabeste wao na ndio maana watu wengi hawatimizangi target zao.Na kaama hukufanikiwa kutimiza target zako za 2016 usikonde, 2017 itakua mwaka wako.


JOIN THE CONVERSATION


next